Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mary Robinson ziarani Burundi

Mary Robinson ziarani Burundi

Burundi imekubali uwanja wake wa ndege utumiwe katika harakati za kijeshi za Jeshi la Umoja wa mataifa mpashariki mwa DR Congo. Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameyatangaza hayo hii leo baada ya kumpokea mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa katika Maziwa Makuu Mary Robinson aliye ziarani katika ukanda huo katika juhudi za kustaawisha mashariki mwa Congo.

Burundi pia imeelezea utayari wake wa kupeleka maafisa wake wa kijeshi kutoa mafunzo kwa brigedi ya Umoja wa Mataifa itakayokwenda Mashariki ya Congo kusimamia amani.

Kutoka Bujumbura, Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga anatuarifu zaidi.