Mexico iache "mabavu" dhidi ya raia wake

3 Mei 2013

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa amesema  serikali ya Mexio inapaswa kuweka bahaya mifumo yake ya utendaji wa kuangalia maeneo bora ya matumizi ya nguvu za dola pasipo kuziendea kinyume haki za binadamu.

Christof  Heyns ameitaka serikali hiyo kujiepusha na matumizi ya nguvu kama vile nguvu za kijeshi wakati inapotekeleza majukumu yake kwani kwa kufanya hivyo kumesababisha mamia ya watu kupoteza uhai wao.

Amesema kuwa ni vyema serikali hiyo ikaangalia upunguzaji wa matumizi ya nguvu za ziada kwani inawajibu wa kulinda na kutetea haki za binadamu.

Ameongeza kuwa kuna utashi uliojitokeza baina ya serikali na vyama vya kiraia vilivyokubaliana haja ya kuweka sheria madhubuti ambazo zitasaidia kukabiliana na uvunjifu wa haki za binadamu na siyo kuendelea kutumia utawala wa kimabavu.