Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanzo cha vifo vya uduvi (shrimps) mwambao wa Asia chajulikana

Chanzo cha vifo vya uduvi (shrimps) mwambao wa Asia chajulikana

Katika hatua kubwa ya kisayansi watafiti kwenye chuo kikuu cha Arizona hapa Marekani wamebaini chanzo cha ugonjwa wa ajabu ambao umekuwa ukiathiri mavuno ya uduvi baraniAsia.

Magonjwa yaliyotajwa kama “vifo vya mapema vya uduvi” EMS na ule unaoathiri mapezi ya uduvi yaani Hepatopancreatic Necrosis kwa zaidi ya miaka miwili vimekuwa vikisababisha vifo vya idadi kubwa ya uduvi katika nchi mbalimbali za Asia ambako watu milioni moja wanatrgemea uvuvi wa uduvi kwa ajili ya maishayaoya kila siku.

Mpaka sasa chanzo cha vifo hivyo kilikuwa kitendawili kisichi na jibu na kusumbua vichwa vya wanasayansi, mamlaka za afya za wanyama na wakulima na hivyo kufanya hatua za kuzuia na kutibu kuwa ngumu saana.

Lakini sasa maradhi yamebainika na yanasababishwa na bacteria ambao hupatikana mara nyingi kwenye maji ya chumvichumvi yanayozunguka pwani kote duniani.