Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanahabari bado waminywa na wakumbwa na vitisho: UM

Wanahabari bado waminywa na wakumbwa na vitisho: UM

Ikiwa leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Umoja wa Mataifa umetaka usalama zaidi kwa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari wa sekta zote kuanzia radio, magazeti, televisheni na mabloga.

Ujumbe wa siku ya leo ni Zungumza bila hofu na uhuru wa kujieleza kupitia vyombo vyote! Lakini bado Umoja wa Mataifa unasema mazingira ni hatarishi, na kwa kufanya hivyo wananchi wananyimwa haki yao ya msingi, ya kupata habari za ukweli na uhakika kutoka vyanzo mbali mbali vya habari.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema uhuru wa kujieleza ni msingi wa utawala bora, maendeleo endelevu na hata amani na usalama wa kudumu duniani, lakini bado inashuhudiwa serikali, kampuni, wahalifu wakitishia waandishi wa habari, na hofu yake ni kwamba, wengi wao hawachukuliwi hatua zozote.

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO linasema mazingira ya kazi ya uandishi yamekuwa salama lakini kwa hivyo karibuni hali imetia wasiwasi.

Elizabeth Kyondo ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO nchini Tanzania.

(SAUTI YA Elizabeth KIONDO)