Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yaendelea kutawanya watu Pakistan:OCHA

Machafuko yaendelea kutawanya watu Pakistan:OCHA

Huko nchini Pakistan katika maeneo ya Kaskazini yanayodhibitiwa na FATA takriban watu 76,000 wamekimbia katika bonde la Tirah tangu katikati ya mwezi Machi kufuatia mapigano yanayoendelea baina ya makundi hasimu yenye silaha na operesheni za majeshi ya serikali dhidi ya makundi hayo.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu misaada na masuala ya kibinadamu OCHA watu hao ambao wamekuwa wakimbizi wa ndani wanahitahji chakula, huduma za afya na ulinzi.

Mashirika ya Umoja wa mataifa na wadau wa misaada ya kibinadamu watoa mahitaji muhimu lakini wanahitaji dola milioni 25 ili kushughulikia ipasavyo mahitaji ya wakimbizi hao wa ndani katika muda uliosalia hadi mwisho wa mwaka.