Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saudi Arabia yakumbwa na virusi vya nCoV:WHO

Saudi Arabia yakumbwa na virusi vya nCoV:WHO

Wizara ya afya nchini Saudia Arabia imeliarifu shirika la afya duniani kwamba imebaini visa vipya saba vya maambukizi ya virusi vijulikanavyo kama novel corona (nCoV) vinavyoshambulia mfumo wa hewa. Virusi hivyo vimesababisha vifo vya watu watano.

Wagonjwa wawili kati ya hao saba hivi sasa wako katika hali mahtuti, na serikali inafanya uchunguzi kujua chanzo cha mlipuko huo.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba sio safari wala maingiliano na wanyama yaliyochangia visa hivyo.

Kuanzia Septemba mwaka 2012 hadi sasa WHO imearifiwa visa 24 vilivyothibitishwa katika maabara kote duniani na vifo 16 vya binadamu kutokana na virusi vhivyo ambavyo hushambulia mfumo wa hewa.

WHO inazichagiza nchi wanachama kuwa makini zaidi kubaini maradhi yanayoshambulia mfumo wa hewa na kutoa taarifa haraka.

Glen Thomas ni msemaji wa WHO

(SAUTI YA GLEN THOMAS)