Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibinadamu yazidi kutetereka DRC:WFP

Hali ya kibinadamu yazidi kutetereka DRC:WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP limesema linatiwa hofu na kuendelea kutetereka kwa hali ya kibinadamu kwenye maeneo ya jimbo la Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kufuatia mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa kundi la Mayi Mayi.  Kwa mujibu wa shirikahilowatu wapatao 200,000 wamelazimika kukimbia eneohilokatika miji mitatu ya Manono, Mitwaba, na Pweto katika mwezi uliopita wa Aprili. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(SAUTI YA ELISABETH BYRS)