Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UM Somalia sasa kuitwa UNSOM

Ujumbe wa UM Somalia sasa kuitwa UNSOM

Hatimaye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloanzisha ujumbe wake wa usaidizi nchiniSomalia, UNSOM utakaochukua nafasi ya ofisi ya kisiasa, UNPOS.  Azimio hilo limepitishwa kwa kauli moja na wajumbe wote ambapo UNSOM itaanzishwa tarehe Tatu mwezi ujao na itahudumu kwa kipindi cha awali cha mwaka mmoja.  Kwa mujibu wa azimio hilo, mamlaka ya ujumbe huo ni pamoja na kutekeleza majukumu ya Umoja wa Mataiaf kwa kusaidia serikali ya Somalia na ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini humo, AMISOM. Halikadhalika ujumbe huo pia utafuatilia na kuripoti kwa Baraza la Usalama ukiukwaji wowote wa haki za binadamu na sheria za kibinadamu za kimataifa, ikiwemo vitendo vyovyote vya ukatili kwa wanawake na watoto nchini Somalia. Mwakilishi wa kudumu waSomaliakatika Umoja wa Mataifa Balozi Elmi Ahmed Duale ameunga mkono azimiohilo.

(SAUTI YA Balozi Duale)

"Naamini azimio hili litahakikisha angalau hatua za awali za usaidizi wa Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama kwa Somalia zitakuwa thabiti hususan pendekezo la UNSOM ambalo litahakikisha Somalia na serikali ya Somalia vitakuwa na mlango mmoja wa mashauriano na usaidizi.”