Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Robinson akutana na Museveni

Robinson akutana na Museveni

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika nchi za  Maziwa makuu Mary Robinson amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Uganda Yower Museveni ,mawaziri na wawakilishi wa asasi za kiraia nchini humo

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema mazungumzo hayo yalilenga katika utekelezaji wa mkakati wa ushirikiakno wa amani na usalama kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC

Nesirky amesema Mwakilishi huyo Maalum wa katibu Mkuu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelekea Burundi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika nchi za maziwa makuu  ambapo pia anatarajiwa kukamilisha ziara yake nchini Afrika Kusini.