Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ajadili Syria na wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama

Ban ajadili Syria na wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama

Katibu Mkuu wa UMoja wa mataifa Ban Ki-moon leo amewaalika wajumbe watano wa kudumu wa baraza la Usalama katika kikao kisicho rasmi kujadili suala la Syria.

Ban na wajumbe hao wamejadili uwezekano wa hatua za kidiplomasia kumaliza mzozo wa Syria, Ban pia amewapa taarifa wajumbe hao kuhusu hatua ilityofikiwa na tume ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali nchini humo.

Mbali na silaha wamezungumzia kuzidi kuzorota kwa hali ya kibinadamuSyriana katika nchi jirani na mwisho juhudi za kimataifa katika kushughulikia matatizo hayo ya kibinadamu.