Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa zaidi vya mafua ya H7N9 kwa binadamu vya bainika China

Visa zaidi vya mafua ya H7N9 kwa binadamu vya bainika China

Tume ya taifa ya afya na uzazi wa mpango nchini Uchina imeliarifu shirika la afya duniani WHO kuhusu kuthibitishwa kwa visa vingine viwili vya maambukizi ya virusi vya mafua ya avian H7N9 kwa binadamu.

Mgonjwa wa kwanza ni mwanaume mwenye umri wa miaka 58 kutoka jimbo la Fujian ambaye alianza kuumwa April 21 mwaka huu na wa pili ni mwanaume wa miaka 69 kutoka jimbo la Hunan aliyeanza kuugua april 23 mwaka huu.

Wagonjwa wengine wawili walioripotiwa awali wamefariki dunia na hivyo kufanya idadi ya visa vilivyothibitishwa kwa binadamu hadi leo kufikia 128 vikiwemo vifo 26 vilivyoripotiwa kwa WHO.

Shirika la afya linasema linafuatilia kwa karibu kuthibitishwa kwa visa hivyo huku serikali ya Uchina ikitekeleza njia za kukika na kuthibiti virusi hivyo katika maeneo yaliyoathirika.

Uchunguzi unaendelea kubaini ukubwa wa tatizo na chanzo cha maambukizi hayo kwa binadamu.

Na hadi pale chanzo kitakapojulikana na kudhibitiwa kuna hofu idadi ya maambukizi itaongezeka.