Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la UM lahitimisha mkutano wa 75

Baraza la UM lahitimisha mkutano wa 75

Baraza la Uongozi la Umoja wa Mataifa ambalo ni kamishna ya fidia, limehitimisha mkutano wake wa 75 ambao pia umewajumuisha wajumbe kutoka nchini Iraq.

Likiwa chini ya urais wa Australia, baraza hilo limejadilia maazimio yaliyofikiwa siku za nyuma ikiwemo azimio lilipitishwa mwaka 2011 ambalo linaweka mkazo juu ya ulinzi wa mazingira.

Wajumbe katika mkutano huo walipongeza maendeleo yaliyofikiwa na nchi za Jordan na Kuwait ambazo zimefaulu kutekeleza kwa kiwango kikubwa maazimio yaliyofikiwa mwaka 2011.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na wajumbe kutoka Jordan, Kuwait na Saudia Arabia umeazimia kuw ana kikao kingine Novemba 19 hadi 21 mwaka huu.