Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waidhinisha ufadhili kwa miradi ya kupambana na uharamia nchini Somalia

UM waidhinisha ufadhili kwa miradi ya kupambana na uharamia nchini Somalia

Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaopambana na uharamia umedhinisha miradi inayokabiliana na uharamia nchini Somalia na maeneo mengine yaliyoathirika yakiwemo Djibouti, Ethiopia, Kenya, Maldives na usheli usheli . Tangazo hilo lilitolewa mjini New York na naibu katibu mkuu kwenye masuala ya kisiasa kwenye Umoja wa Mataifa Tayé-Brook Zerihoun ambaye anasisimia bodi inayounga mkono miradi ya kukabilina na uharamia pwani mwa Somalia.

Bwana Zerihoun anasema kuwa kupungua kwa visa vya uharamia ni ishara ya mafanikio ya Umoja wa Mataifa , mashirika ya kimataifa na wale walio kwenye sekta ya usafiri wa bahari. Miradi hiyo mitano iliyoidhinishwa na inayogharimu dola milioni mbili inalenga kuhakikisha kuwa kesi zinazohusu uharamia zinazoendela zinafanyika kwa njia ya haki na kuwa haki za binadamu , afya na usalama kwa wanaokabiliwa na kesi hizo vimelindwa.