Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msumbiji yajadili mikakati ya vivutio vya uwekezaji nchini mwake:

Msumbiji yajadili mikakati ya vivutio vya uwekezaji nchini mwake:

Ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Msumbiji umeieleza tume ya Umoja wa mataifa inayohusika na uwekezaji na maendeleo kwamba serikali yake inaunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na tathimini ya UNCTAD kuhusu sera nchini humo na kuitaka pamoja na mambo mengine kufanya mabadiliko ya sheria zake za uwekezaji. Kama inavyoeleza ripoti ya Alice Kariuki.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Akiwasilisha ripoti ya sera za uwekezaji kwa ajili ya kufanyiwa tathimini, naibu waziri wa mipango na maendeleo wa Msumbiji Amelia Nakhare ameiambia tume ya tathimini ya Umoja wa mataifa kwamba tathimini yao ni muhimu sana ukizingatia hali halisi ya uchumi wa Msumbiji .

Amesema mapendekezo ya tume hiyo yataisaidia nchi yake kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji hususani binafsi ili kuchagiza maendeleo ya kijaa na kiuchumi.

James Zhan mkurugenzi wa UNCTAD kitengo cha uwekezaji amesema tume imebaini maeneo mbalimbali ambayo yanahitaji kushughulikiwa nchini Msumbiji ili kuvutia tena uwekezaji.

Imependekeza nchi hiyo kulenga uwekezaji wa moja kwa moja toka nje ambao utasaidia kuongeza ajira kwa watu wa Msumbiji na kupanua wigo wa maendeleo ya kiuchumi katika sekta mbalimbali, kuimarisha sheria za uwekezaji, na kuboresha miundo mbinu.