Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msimu wa uhaba wa chakula Sudan Kusini waongeza ukosefu wa uhakika wa chakula

Msimu wa uhaba wa chakula Sudan Kusini waongeza ukosefu wa uhakika wa chakula

Nchini Sudan Kusini, kuzorota kwa upatikanaji wa chakula kunazidi kuchochewa na kuendelea kwa msimu wa uhaba wa bidhaa. Habari zinasema bei za vyakula zimepanda, kiwango cha kipato kimeporoka na kwamba ukosefu wa usalama unafanya watu washindwe kushiriki katika shughuli za kujipatia kipato kama anavyoripoti George Njogopa.

(RIPOTI YA GEORGE)

Mamia ya watu waliokosa makazi katika jimbo la Jonglei wanaripotiwa kuwa katika hali ngumu zaidi na kunashuhudiwa kuzorota kwa shughuli za utoaji misaada ya usamaria mwema kutokana na eneo hilo kuendelea kuwa tete kwa usalama.

Bei ya bidhaa ikiwemo vyakula na mahitaji mengine muhimu imeendelea kuwa juu hali ambayo imewaathiri wananchi wengi wanaotegemea bidhaa za sokoni.

Bei hizo zinaripotiwa kupanda kwa zaidi ya mara tano na kunawasiwasi ikaendelea kupanda zaidi katika msimu wa mwezi May na Julai. Pamoja na kwamba hali ya kibiashara baina ya Sudan Kusin na Sudan ikitegemewa kuimarika, lakini kwa wananchi wa kawaida bado wataendelea kuwa katika mazingira magumu.

Vikwazo vya kibiashara pamoja na marufuku ya uhamiaji ni baadhi ya sababu ilifanya familia nyingi kukosa vyanzo vya mapato jambo ambalo athari yake imeanza kujitokeza kwenye chakula.