Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Togo kuongoza baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Mei

Togo kuongoza baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Mei

Nchi ya Togo inatarajia kuchukua nafasi ya uraisi wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwezi huu wa May, ikichukua nafasi hiyo baada yaRwandakumaliza muda wake.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Umoja wa Matifa Martin Nesirky amesema Mwakilishi wa kudumu wa Togo katika Umoja wa Mataifa  Balozi Kodjo Menan anatarajiwa kuelezea mpango wa Baraza hilo kwa mwezi May hapo kesho.

Rwandailiongoza nafasi ya uraisi wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi April ambapo katika kipindi hicho cha uongozi wake barazahilolilijielekeza zaidi katika suluhu za migogoro hususani barani Afrika.