Baraza la Haki za binadamu lapata ripoti kuhusu Cameroon

1 Mei 2013

Baraza la Haki za  binadamu  linaloendelea na kikao chake huko Geneva, limepata ripoti kuhusu masuala ya haki za binadamu huko Cameroon. Alice Kariuki anafafanua zaidi.

 (TAARIFA YA ALICE)

Baraza la Haki za Binadamu limekutana leo asubuhi kujadili hali ya haki za binadamu nchini Cameroon. Wajumbe wa baraza hilo wamesifu maendeleo yaliopatikana katika masuala mbali mbali yakiwemo hatua za kushughulikia hali ya kutojali na kuwajibisha viongozi ambao wanukiuka haki za binadamu.

Hata hivyo wametoa mapendekezo kwa Cameroon kuongeza juhudi za kukabiliana na masuala kama ukeketaji, kuweka sera za kuondokana na aina zote za ubagudi dhidi ya wanawake, na kuhakikisha uwepo wa uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari.

Naye mkuu wa ujumbe wa Cameroon katika kauli yake amesema nchi yake imechukua hatua muhimu za kuimarisha hali ya haki za binadamu zikiwemo zile za watu kufanya kazi.

(SAUTI YA MKUU WA UJUMBE WA CAMEROON)

Kuhusu haki ya kufanya kazi na upatikanaji wa ajira, nchi ya Cameroon imeanzisha Februari 2011 mpango muhimu wa kuandiksha vijana 25,000 katika sekta ya umma.

Serikali pia inajivunia kwamba mwaka 2012, mbali na ajirz zisizo rasmi, ajira nyingine 160,000 zimepatikana kutokana na uchumi wa kisasa.