Maandalizi ni muhimu katika kukabili majanga:ESCAP

1 Mei 2013

Maandalizi kwa ajili ya zahma, hasa majanga ya asili na mdororo wa kiuchumi lazima iwe kitovu kwa ajili ya mipango ya maendeleo katika kanda yaAsiana Pacific ambayo imekuwa katika tishio kubwa la kukabiliwa na majanga . 

Hayo yamejadiliwa na mameneja wa kukabili majanga kwenye kongamano la Umoja wa mataifa linalohusisha nchi za Asia Pacific huko Bangkok Thailand.

Wataalamu wa majanga na matatizo ya kiuchumi kutoka jumuiya za mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) ambazo ni Indonesia, Pakistan na Ufilipino wakizungumza kwenye kongamano hilo la 60 la tume ya Umoja wa mataifa ya uchumi na jamii kwa nchi Asia na Pacific ESCAP wamekubaliana kwamba  uwezo wa kukabili majanga hayo unatokana na maandalizi mazuri.

Naye mkuuwa ESCAP Dr. Noeleen Heyzer amesisitiza kwamba jambo mla kwanza serikali lazima ziwekeze katika kuzuia na maandalizi, kwani ni muhimu na ni gharama nafuu kuliko zile za kukabili athari. Amesema kinachohitajika ni kuweka sera muafaka na ufuatiliaji.