Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vurugu za Iraq zamsikitisha Ban, atuma salamu za rambirambi kwa wafiwa

Vurugu za Iraq zamsikitisha Ban, atuma salamu za rambirambi kwa wafiwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza masikitiko yake juu ya ongezeko la matukio ya ghasia nchini Iraq yaliyosababisha vifo vya watu wengi na mamia kujeruhiwa. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu imemkariri Bwana Ban akituma rambirambi kwa wafiwa wa matukio hayo ya wiki iliyopita na kuwatakia majeruhi ahueni ya haraka. Halikadhalika ametoa wito kwa vikosi vya usalama nchiniIraqkujizuia ipasavyo wanaporejesha utulivu huku pia akiwataka waandamanaji kutekeleza haki ya kuandamana kwa amani. Hata hivyo Bwana Ban ameeleza wasiwasi wake juu ya uamuzi wa kufuta leseni za vituo kadhaa vya televisheni nchini Iraq na kutaka mamlaka husika kufikiria upya uamuzi huo huku akiwakumbusha kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni msingi wa demokrasia. Ametaka viongozi wote nchini Iraqkukaa pamoja na kufanya majadiliano ya dhati kwa lengo moja la kumaliza mzozo wa kisiasa unaokumba nchi hiyo huku akiwahakikishia kuwa Umoja wa Matifa kupitia ofisi yake UNAMI iko tayari kusaidia nchi hiyo na wananchi wake kujenga amani, demokrasia na ustawi.