Bi Robinson ahitimisha ziara DRC

30 Aprili 2013

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda wa Maziwa Makuu, Bi Mary Robinson, ambaye amehitimisha ziara yake katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC hii leo, amesema kuwa umuhimu wa ziara yake nchini humo imekuwa ni kusikiliza na kuwa na mazungumzo ya wazi na pande zote husika, ili kuhakikisha makubaliano ya kuleta amani DRC yanatekelezwa.

Bi Robinson amekuwa na mazungumzo na Rais Kabila, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje, mashirika yasiyo ya kiserikali, MONUSCO, wanaharakati wa haki za binadamu, pamoja na vikundi via wanawake na via kidini. Mwishoni mwa ziara yake, Bi Robinson amezungumza na mwandishi habari wa Radio Okapi,  Alain Irung

(SAUTI YA ROBINSON)

Akijibu suali kuhusu mazungumzo yake na mamlaka ya DRC Bi Robinson amesema:

(SAUTI YA BI ROBINSON)

Ziara ya Bi Robinson itampeleka pia Rwanda,Uganda,Burundi, Afrika Kusini na kuhitimishwa Ethiopia, kwenye makao makuu ya Muungano wa Afrika.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter