Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaendesha mafunzo kwa wafanyabiashara wadogo wa Ethiopia

IOM yaendesha mafunzo kwa wafanyabiashara wadogo wa Ethiopia

Shirika la kimataifa linalohusika na uhamiajI IOM, limefanikisha mpango wa utoaji mafunzo ya kibiashara kwa raia wa Ethiopia waliorejea nchini humo kwa hiari kutoka Misri na Libya

Mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tano yaliwaleta pamoja wahitimu 26,ambao walipewa ujuzi katika maeneo ya ujasiria mali na mbinu za uanishwaji wa biashara.

Akizungumzia mafunzo hayo, afisa wa IOM nchin Ethiopia Abraham Tamrat amesema kuwa wahitimu sasa wapo kwenye mkondo mzuri wa kuanzisha biashara .

Mafunzo hayo yameanzishwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya IOM na mpango wa kuwapiga jeki raia wa Ethiopia walikuwa nchini Misri na Libya ambao kwa sasa wameamua kurejea nyumbani kwa hiari.