Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO kupeleka ujumbe Bangladesh kufuatia kuporomoka kwa jingo la Rana Plaza

ILO kupeleka ujumbe Bangladesh kufuatia kuporomoka kwa jingo la Rana Plaza

Shirika la kazi duniani ILO linatapeleka ujumbe wa ngazi za juu nchini Bangladesh katika siku chache zijazo ili kusaidia na kuharakisha hatua za kila upande zinazohitajika kufuatia kuporomoka kwa jingo laRana Plaza mjini Savar lililokatili maisha ya watu 380 na wengine wengi kujeruhiwa.Ujumbe huo utaongozwa na naibu mkurugenzi mkuu wa ILO anayehusika na operesheni za nje Gilbert Houngbo.

Mkurugenzi mkuu wa ILO Guy Ryder amesema anamwandikia waziri mkuu wa Bangladesha Sheikh Hasina akimtaka kuchukua hatua mara moja kuzuia tukio kamahilokutokea tena, zahma ambayo inaweza kuzuilika katika maeneo ya kazi.

ILO inasema mpango maalumu lazima ujumuishe ukabiliane na viwanda vibovu kwa kwa kuvihamiashia penye usalama na kuboresha miundombinu, kuanzisha ukaguzi katika maeneo ya kazi , serikali kujidhatiti katika kutekeleza sheria na misingi ya kazi, kuchagiza mazungumzo ya afya na usalama kazini, na kupitisha sheria ya kazi itakayohakikisha haki za shirika na wafanyakazi kwa kuzingatia sheria na misingi ya ILO.