Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha mazungumzo ya kumaliza uhasama, Iraq, Kurdistan

UM wakaribisha mazungumzo ya kumaliza uhasama, Iraq, Kurdistan

Iraq na Kurdistan zimeanzisha majadiliano kwa shabaha ya kumaliza mivutano ya muda mrefu huku Umoja wa Mataifa ukiamini kupatikana kwa suluhu ya kudumu.

Maafisa wa pande zote mbili wamekutana kabla ya mawaziri wakuu kuwa na mkutano wao siku ya jumanne, mjini Bagdad.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler UNAMI amesema kuwa, mkutano huo utakaowaleta pamoja waziri mkuu Nuri-al-Maliki na mwenzio Nichervan Barzani,utafungua njia kumaliza mivutano ya muda mrefu,

Pande hizo zimekuwa zikitofautiana kwenye maeneo mbalimbali, hivyo kukubali kwa viongozi wake kuwa na majadiliano ya mezani ni ishara ya utunzuaji wa hitilafu hizo.