Skip to main content

Syria iruhusu uchunguzi katika madai ya kutumika silaha za kemikali: Ban

Syria iruhusu uchunguzi katika madai ya kutumika silaha za kemikali: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameitaka serikali ya Syria iruhusu uchunguzi wa madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini humo bila kuchelewa na bila masharti. Joshua mmali na maelezo zaidi

(PKG JOSHUA MMALI)

Akiandamana na mtaalam msimamizi wa timu ya uchunguzi huo, Dr. Åke Sellström, Bwana Ban amewaambia waandishi wa habari mjiniNew York, kuwa ili kuweza kuchunguza kikamilifu madai ya matumizi ya silaha za kemikali na kuondoa wasiwasi, timu hiyo inatakiwa iwezeshwe kuyafikia moja kwa moja maeneo ambako silaha za kemikali zimedaiwa kutumika.

Ban amesema huu ni wakati muhimu katika juhudi zetu kuipeleka timu yetu kutekeleza majukumu yake.

"Uchunguzi wa kina na wa kuaminika unahitaji uwezo wa kuyafikia maeneo yote ambako silaha za kemikali zimedaiwa kutumika. Leo April 29 ni siku ya kuwakumbuka wahanga wa vita vya silaha za kemikali. Wakati tukikabiliana na madai haya, nawahimiza wote wanaohusika kutimiza wajibu wao katika kutuwezesha kudhibiti vyema silaha hizi mbovu.”