Brazil yatoa msaada mkubwa wa chakula kwa wapalestina

Brazil yatoa msaada mkubwa wa chakula kwa wapalestina

Jimbo la Brazil ambalo ni mzalishaji mkubwa wa mpungua la Rio Grande do Sul, kupitia serikali kuu limetoa msaada wa tani 11.500 za mchele kwa shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

Tangazo la msaada huo limetolewa na gavana wa Rio Grande do Sul, bwana Tarso Gerno mjini Jerusalem kwenye kambi ya wakimbizi ya Shufaat

. Gavana huyo amesema amefurahi kujumika na wakimbizi hao wa Kipalestina ambao watafaidika na msaada huo wa chakula. Ameongeza kuwa ameklwenda Jerusalem kwani ilikuwa muhimu kujionea mwenyewe adha inayowakabili wakimbizi hao katika aeneo linalodhibitriwa na Israel. Amesema katika siku za usoni anashirikiana kwa karibu na serikali kuu ya Brazil kufungua kituo maalumu kwenye aneo la Pelotas karibu na mashamba yanayozalisha mpunga ili kurahisisha usafirishaji wa msaada huo kwenye kwa UNRWA. Msaada huo unatosheleza mahitaji ya chakula kwa wakimbizi kwa Kipalestina kwa kipindi cha mwaka mzima, na utasambazwa katika maeneo yote ya Wapalestina yanayokaliwa ikiwemo Gaza na Ukingo wa Magharibi lakini pia Jordan, Lebanon na Syria.