Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na washirika kusaidia kuboresha elimu kwa wote

UNESCO na washirika kusaidia kuboresha elimu kwa wote

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ambalo limetiliana saini na shirika linalohusika na elimu ya msingi Educate A Child for Quality Primary Education kwa lengo la kufanikisha lengo la milenia la elimu kwa wote. Makubaliano yametiwa saini leo hukoDoha kama anavyoripoti George Njogopa.(TAARIFA YA GEORGE)

Ushirikiano huo unalenga kutoa msukumo kwa sekretarieti inayotoa kipaumbele cha elimu .Sekretatieti hiyo inayofahamika kwa kimombo Global Education First Initiative, (GEFI) ilizinduliwa rasmi na Katibu Mkuu Ban Ki-moon mwezi Septemba mwaka jana.

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema utendaji kazi wa sekretarieti hiyo sasa umepata msukumo mpya, msukumo ambao utaiwezesha sekretarieti hiyo kuwa na uwanja mpana wa kushughulikia mambo yanayohusu haki ya kupata elimu.

Ama ameeleza sekretarieti hiyo sasa itakuwa na fursa ya kuweka mikakati ambayo itafanikisha agenda ya kumsaidia mtoto kupata elimu bora.

Amesema kuwa ikiwa kumesaliwa na siyo zaidi ya siku 1,000 ili kufikia malengo ya maendeleo ya mellenia , dunia inapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kuzibainisha na kuzifanyika kazi changamoto zinazokwaza baadhi ya watoto kutofikiwa na elimu.