UM watenga fedha za kukabiliana na hali mbaya ya kibindamu Chad

26 Aprili 2013

Shirika la UM la kuratibu misaada ya kibinadamu (OCHA) limesema kuwa UM umetenga dola milioni tano za kukabiliana na hali mbaya ya kibinamadu nchini Chad. Fedha hizo zitatumika kukidhi mahitaji ya dharura ya wakimbizi wa Sudan na wahamiaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA JENS LAERKE)

Fedha hizo hasa zitatumiwa kutoa ulinzi kwa wakimbizi, msaada wa chakula na kusaidia jamii zinazoishi katika mazingira magumu. Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Chad amesema msaada huo umefika wakati mashirika ya misaada ya kibinadamu yanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa fedha na utasaidia kukidhi mahitaji muhimu ya zaidi ya wakimbizi 30,000 kutoka Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati na pia zaidi ya raia 19,000 wa Chad wanaorudi kutoka Sudan.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter