Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto, Burundi yapiga hatua kumstawisha mwanamke

Licha ya changamoto, Burundi yapiga hatua kumstawisha mwanamke

Ikiwa zimesalia chini ya siku Elfu Moja kabla ya ukomo wa Malengo ya Milenia mwezi Disemba mwaka 2015, Burundi  yaelezwa kuwa imepiga hatua kubwa katika  moja wapo ya malengo hayo hususan lile la usawa wa kijinsia kwa kuweka mazingira ya usawa kati ya wanawake na wanaume katika Nyanja mbali mbali. Katiba ya nchi hiyo imewatengea wanawake kwa uchache asilimia 30 ya uwakilishi kwenye taasisi za uongozi wa taifa  na kuifanya nchi hiyo kuorodheshwa nafasi ya nne ulimwenguni kama taifa lilowapa wanawake nyadhifa muhimu serikalini. Pamoja na mafanikio   hayo ya kujivunia ,  bado kuna changamoto mathalani kuwafikia na kuwawezesha wanawake wa vijijini  na wale ambao hawakubahatika kusoma ili kuwaondoa katika lindi la umasikini na dhulma mbalimbali. Je nini kimefanyika na nini kinafanyika? Basi Ungana na mwandishi wetu wa maziwa Makuu RAamdhani Kibuga katika makala haya