Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kuwezesha wasomali walioko Uingereza kuchangia maendeleo ya nchi yao

IOM kuwezesha wasomali walioko Uingereza kuchangia maendeleo ya nchi yao

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kuwawezesha wahamiaji wa kisomali nchini Uingereza kushiriki maendeleo ya nchi yao kama anavyo ripoti Alice Kariuki.

 (RIPOTI YA ALICE)

Wahamiaji hao wa kisomali walioko Uingereza watapatiwa mafunzo na IOM kwa lengo la kusaidia ustawi wa uchumi wa nchi yao ambayo kwa miongo kadhaa imekuwa katika migogoro. 

Hatua hiyo  ya IOM inakusudia kutumia ujuzi wa Wasomali katika nyanja kama vile elimu na afya na hiyo ni sehemu ya mkakati wa awali wa IOM wa kutumia ujuzi wa wahamiaji wa Afrika wanaoishi ughaibuni ili kuleta maendeleo katika nchi zao. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE)