Skip to main content

Wakimbizi kutoka Syria ni mzigo mkubwa kwa UNHCR na majirani zake

Wakimbizi kutoka Syria ni mzigo mkubwa kwa UNHCR na majirani zake

 Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR laeleza  kuzidiwa uwezo wa kutoa huduma za tiba kwa wakimbizi wa  Syria kama anavyoeleza  Jason nyakundi.  (PKG YA JASON NYAKUNDI)Kukiwa na zaidi ya wakimbizi milioni moja nchini Iraq, Jordan na Lebanon shughuli za utoaji huduma za kiaya kwenye nchi hizi zimekumbwa na changamoto kutokana  na kuongezeka idadi ya wakimbizi wanaotafuta huduma za afya.

UNHCR inasema kuwa hali hiyo imechochewa na ukosefu wa uwezo  wa mashirika ya misaada kutoa huduma za afya kutokana na ufadhili mdogo.

Ripoti hiyo inasema kuwa wakimbizi walio na magonjwa sugu kama kisukari, ugonjwa wa moyo kupiga kwa kasi na mengineyo hawapati matibabu yaliyo mazuri hasa wale walio nje ya kambi. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTO YA ADRIAN EDWARD)

“Tunaendelea na washirika wetu , kutoa huduma za afya kwa wakimbizi kwenye kambi nchini Jordan na Iraq. Lakini kwa wakimbizi wanaoishi nje ya kambi hasa mijini hali ni ngumu zaidi. Nchini Jordan na Iraq huduma za  matibabu zinasimamiwa na serikali , UNHCR na mashirika mengine lakini utoaji wa matibabu kama vile upasuaji na matibabu ya saratani inakuwa vigumu. Nchini Lebanon mifumo mingi ya kifya imebinafsishwa. ukosefu wa huduma unamaanisha kuwa sisi na washirika wetu tutapunguza huduma ghali za kiafya.”

UNHCR inasema kuwa idadi ya wakimbizi wa Syria waliosajiliwa katika eneo hilo imefikia watu milioni 1.4