Ban azungumza na Rais wa Equatorial Guinea

26 Aprili 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Rais Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial  Guinea ambapo amemshukuru Rais nguema mwa mchango wake katika utatuzi wa mizozo kwa njia ya amani barani afrika. Viongozi hao  wawili walijadiliana kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Umoja wa Mataifa na taifa la Equatorial Guinea na jitihada wanazofanya kutimiza malengo ya maendelo ya milenia. Ban  alisema kuwa Umoja wa Mataifa umejitolea kusaidia katika utatuzi kwa njia ya amani  tofauti za mpaka kati ya Equatorial Guinea na   Gabon. Wawili hao pia walizungumzia mkutano wa 36 wa mawaziri kuhusu usalama katika eneo la Afrika ya kati ambapo Rais Nguma alisema kuwa taifa lake liko tayari katika kuandaa mkutano huo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter