Ban azungumzia taarifa za Marekani kuhusu silaha za kemikali Syria

26 Aprili 2013

Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ana taarifa juu ya barua ambayo Ikulu ya Marekani imewasilisha katika baraza la Kongresi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.  Bwana Ban anachukulia kwa umakini taarifa hizo lakini Umoja wa Mataifa hauwezi kutoa maoni yoyote kwa kuzingatia upelelezi uliofanywa na taifa fulani. Badala washauri waandamizi wa Umoja wa Mataifa wanawasiliana na mamlaka za Marekani juu ya taarifa hizo na kwamba jopo la uchunguzi lililoundwa na Bwana Ban kwenda Syria kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali liko tayari na litaondoka kati ya saa 24 au 48 zijazo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter