Zaidi ya wakimbizi 30,000 wamewasili nchini Yemeni ndani ya mwaka huu

26 Aprili 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limesema kuwa kiasi cha wakimbizi na wahamiaji 30,000 wamewasili nchini Yemen hadi kufikia sasa.

Wengi wa wahamiaji hao wanaripotiwa ni wenye uraia wa Ethiopia na kiasi kidogo ni kutoka Somalia. Pia kuna wengine kutoka nchi kadhaa za kiafrika.

UHHCR inasema kuwa, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi sasa kuna jumla ya wahamiaji 477,000 ambao wamewasili nchini humo wengi wao wakitumia usafiri wa mashua wakitokea katika eneo la Pembe ya Afrika

Wakati makundi mengine yanayoingia nchini humo yakihesabiwa kama wahamiaji wengine ni wale wanaosaka hifadhi, lakini raia wanaotoka nchini Somalia wanahesabiwa kama wakimbizi.

Kukosekana kwa hali ya utengamano wa kisiasa na mizozo inayoendelea kuikumba Yemen imekuwa vigumu kwa mamlaka nchini humu kudhibiti makundi ya wahamiaji wanaomiminika kwa wingi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter