Baraza la Usalama laamuru ujumbe wa kuweka udhibiti Mali, MINUSMA

25 Aprili 2013

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha mswada unaoamuru kupelekwa vikosi vya kulinda amani nchini Mali, na kubadilishwa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo kuwa ujumbe wenye umbo mseto wa kuimarisha udhibiti, MINUSMA, ambao utahitajika kuanza kajukumu yake mnamo tarehe 1 Julai mwaka 2013. Joshua Mmali na taarifa kamili

 (TAARIFA YA JOSHUA MMALI)

Tarehe hiyo ya Julai mosi huenda ikabadilishwa katika siku 60 zijazo ikiwa Baraza la Usalama litaamua kufanya hivyo, kutokana na hali ya usalama katika eneo la operesheni za MINUSMA.

Ujumbe huo wa MINUSMA, ambao utachukua nafasi ya jumbe wa kimataifa unaoongozwa na Afrika, AFISMA, utakuwa na wanajeshi 11, 200 pamoja na askari polisi 1, 440.

Baraza la Usalama limetoa wito kwa nchi wanachama kuchangia vikosi hivyo vya wanajeshi na polisi, ambao watasaidia kufanikisha majukumu ya MINUSMA, na pia ziendelee kuisaidia AFISMA, hadi hapo MINUSMA itakapoanza majukumu yake.

 Baraza hilo pia limetoa wito wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon kumteua haraka Mwakilishi Maalum kuhusu Mali na Mkuu wa MINUSMA, ambaye atakuwa na mamlaka ya kuratibu majukumu na operesheni zote za MINUSMA.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Uber Coulibaly amelishukuru Baraza la Usalama kwa azimio hilo akisema

 (SAUTI YA COULIBALY)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter