Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO , UNICEF wazindua mpango wa kuangamiza ugonjwa wa polio

WHO , UNICEF wazindua mpango wa kuangamiza ugonjwa wa polio

Shirika la Afya Duniani WHO kwa ushirikino na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF wameibuka na mkakati wa  miaka sita wenye lengo la kuangamiza ugonjwa wa polio

Mpango huu unalenga kutoa chanjo hasa nchini Afghanistan, Pakistan na Nigeria ambapo visa vya ugonjwa huu viko juu. Jason Nyakundi ameandaa taarifa hii

(PKG YA JASON NYAKUNDI)

WHO inasema kuwa idadi ya watoto wanaolemazwa na polio ni vya chini vikiripotiwa visa 19 mwaka 2013 ikilinganishwa na visa 223 vilivyoripotiwa mwaka uliopita.

WHO na UNICEF zinasema kuwa mpango huo ambao unang’oa nanga mwaka huu na kukamilika mwaka 2018 unahitaji dola bilioni 5.5 kutimizwa  huku washirika kadha wakitoa ahadi ya dola bilioni nne.

Kwenye mkutano uliondaliwa mjini Abu Dhabi viongozi walielezea matumaniyaokuwa mpango unasaidia kungamiza ugonjwa wa polio.

Sona Bari ni msemaji wa mpango wa kimataifa wa kuangamiza ugonjwa wa polio.

 “Mpango huu unafanikishwa kutokana na hatua ambazo zimepigwa miaka miwili iliyopita, India ikabaki bila ugonjwa wa polio- ilikuwa nchi ambayo kila mmoja aliiona kuwa vigumu kuangamzia polio na kuendelea kwa nchi tatu zilizosalia. Tunaweza kungalia historia kuhusu jinsi watoto walivyolemazwa na polio miaka 25 iliyopita takriban watoto 350,000. Mwaka huu tumekuwa na watoto 19 waliolemazwa na polio. Haya ni mafanikio makubwa. Hata hivyo kwa kuondoa tunahitajia kufika sufuri. Kwa hivyo kile tunacholenga kufanya ni kuzuia kusambaa kwa virusi hivi kwa miaka miwili inayokuja na kuendelea kufanya utafiti kutafuta plio kila sehemu ya dunia kwa miaka mitatu kuhakikisha kuwa hakuna polio na virusi hivyo vimeangamizwa.”

Polio ni ugonjwa wa kulemaza na unaouwa. Polio inaweza kuvamia wakati wa umri wowote lakini mara nyingi huathiri watoto walio chini ya miaka mitano.