Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Somalia waanza kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa hatari

Watoto Somalia waanza kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa hatari

Serikali ya Somalia imezindua utoaji wa chanjo yenye mchanganyiko wa kinga dhidi ya magonjwa matano hatari kwa watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja na hivyo kuokoa maisha ya maelfu ya watoto.  Chanjo hiyo ni kinga kwa magonjwa kama vile dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini aina ya B na numonia na itakuwa inatolewa chini ya mpango wa chanjo chini Somalia. Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la watoto UNICEF la afya, WHO na ushirikiano wa kimataifa wa chanjo, GAVI yamewezesha kupatikana kwa dozi zaidi ya Milioni Moja kwa mwaka huu kwa ajili ya watoto Laki Nne na Elfu Ishirini na watano, na kila mtoto anatakiwa kupata chanjo hiyo mara tatu.