Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani maziwa makuu barani Afrika kumulikwa wakati wa ziara ya Mary Robinson

Amani maziwa makuu barani Afrika kumulikwa wakati wa ziara ya Mary Robinson

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Maziwa Makuu barani Afrika, Mary Robinson atakuwa na ziara ya wiki moja kwenye ukanda huo kuanzia tarehe 29 mwezi huu.  Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky amewaambia waaandishi wa habari mjiniNew York, kuwa ziara hiyo ya kwanza kufanywa na Bi. Robinson akiwa na wadhifa huo itaanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC,Rwanda,Uganda,Burundina Afrika kusini na hatimaye makao makuu ya Umoja wa Afrika, mjiniAddis Ababa,Ethiopia.   Wakati wa ziara hiyo Bi. Robinson atakuwa na mazungumzo na wawakilishi wa taasisi za kikanda na wajumbe wanaohusika na masuala ya ukanda wa maziwa makuu pamoja na makundi mbali mbali ikiwemo ya wanawake na wabia wa kimataifa.

 

(SAUTI YA MARTIN)

“Mjumbe huyo maalum ataanzisha majadiliano na viongozi wa nchi muhimu kuhusu jinsi ya kuona makubaliano ya hivi karibuni ya amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na eneo hilo  yanaanza kutekelezwa kwa vitendo na ushirikiano ili kumaliza kujirudia mara kwa mara kwa ghasia na mateso huko DRC”