Chanjo ni njia bora na rahisi kulinda maisha ya watoto:Ban

24 Aprili 2013

 

Wiki ya chanjo duniani  ni fursa muhimu ya kuchagiza jamii kuhusu haja ya kuwalinda watoto kutokana na chanjo dhidi ya magonjwa yanayozuilikakamapolio, surua na pepo punda.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe maalumu wa wiki ya chanjo duniani kwenye hafla iliyoandaliwa na  Pan American Health Organization hukoBelize.

Ban ameongeza kuwa chanjo ni moja ya njia bora nay a gharama nafuu katika kulinda maisha ya watoto, kwani amesema hakuna zawadi nzurikamaafya njema katika mwanzo wa maisha ya watoto.

Pia amesema dunia inaweza kusheherekea ukweli kwamba asilimia 80 ya watoto wote ambayo ni zaidi ya wakati mwingine wowote katika historia wamepata chanjo.

Lakini wakati huohuo ameongeza kuwa bado kuna mamilioni ambao wameachwa nyuma wakiishi katika umasikini, bila huduma muhimu, kwenye maeneo ya migogoro na jamii zilizotengwa.

Amesema juhudi za chanjo zimewafikiwa watoto wanne kati ya kila watoto watano kote duniani, akiongeza kwamba sasa ni wakati wa kumfikia huyo mtoto mmoja wa tano popote alipo.

 Amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kwamba kwa pamoja dunia imefungua mlango wa gfursa ya kumaliza maradhikamapolio daima.