Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asia-Pasific kinara wa matumizi ya malighafi -UNEP

Asia-Pasific kinara wa matumizi ya malighafi -UNEP

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP, inaonyesha ukanda wa Asia- Pasific unaongoza duniani kwa matumizi ya malighafi na kwamba utaendelea kuwa kinara katika matumizi hayo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo, uwiano wa biashara katika ukanda wa Asia-Pacific unaonyesha kwamba kiwango cha sasa cha matumizi ya rasilimali hakitoshi kusaidia ukuaji wa uchumi na kubadilisha mfumo wa maisha katika ukanda huo

Mathalani ripoti inaonyesha kwamba kuanzia mwaka 1978 hadi 2008 kumekuwa na ongezeko la ujenzi wa sekta ya madini, na viwanda jambo linaloonyehsa kwamba ukanda huu utakuwa tegemezi kwa kuagiza bidhaa na hivyo kushindwa kuinua uchumi na kuboresha maisha.

Kiwango hicho cha matumizi kadhalika kinaelezwa kuwa na athari mbaya kwa mazingira.