Bahrain yafuta ziara ya mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji

24 Aprili 2013

Matarajio ya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya utesaji Juan E. Méndez kufanya ziara ya uchunguzi hukoBahrain  kuanzia tarehe Nane mwezi ujao yamepeperuka baada ya serikali ya nchi hiyo kuamua kuahirisha ziara yake kamaanavyoripoti George Njogopa.

Hii ni mara ya pili kukatishwa kwa ziara ya mtaalamu huyo na yeye mwenyewe amesema kuwa pamoja na kupokea taarifa ya ghala lakini hakuelezwa zaidi ni lini kunaweza kukapangwa ziara nyingine kwa ajili ya kujadilia mpango wa amani wa nchi hiyo baada ya kuandamwa kwa makundi ya kutetea haki za binadamu na kubinywa uhuru wa kukusanyika.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na serikali inakuja katika kipindi cha wiki moja tu ambacho kilishuhudia askari polisi wakiwaandama vikali waandamanaji walijitokeza bara barani kushinikiza kutolewa ripoti inayowahusu maafisa wa serikali ambao wanadaiwa kuwa nyuma ya vitendo vya utesaji vilivyofanyika mwaka 2011 ambao hadi sasa hawajachukuliwa hatua zozote.

Katika taarifa yake iliyowasilishwa kwa mtaalamu huyo mjini New York, Serikali ya Bahrain imesema kuwa duru la majadiliano linaloendelea sasa, limechukua muda mrefu katika hali isiyotarajiwa hivyo kufanyika kwa ziara hiyo kungeharibu majadiliwa ya majadiliano hayo.