Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yachukua hatua kudhibiti usugu wa dawa dhidi ya Malaria

WHO yachukua hatua kudhibiti usugu wa dawa dhidi ya Malaria

Wakati dunia kesho inaadhimisha siku ya Malaria duniani, Shirika la afya duniani, WHO pamoja na kutambua mafanikio ya kukinga na kudhibiti malaria kwenye nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, limeamua kuangazia usugu wa dawa za Malaria huko ukanda wa Kusini Mashariki mwa Asia eneo la Mekong kama anavyofafanua Dr Thomas Teuscher chanjo ya malaria pia bado ni tatizo. Kwa taarifa zaidi huyu hapa Jason Nyakundi.

(SAUTI YA JASON)

Katika miaka ya hivi karibuni nchi zikiwemo zile zilizo kusini mwa jangwa la sahara zimepiga hatua kubwa katika kupunguza  visa vya ugonjwa wa malaria na kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huu.

Naibu mkurugenzi katika masuala yanayohusiana na HIV , kifua kikuu na malaria kwenye shirika la afya duniani  WHO Dr Hiroki Nakatani hata hivyo anasema kuwa hatua zilizopigwa huenda zikawa kwenye hatari hasa kusini mashariki mwa Asia ambapo ugonjwa huu unaonekana kuwa sugu kwa madawa fulani.

Usugu wa ugonjwa wa Malaria ulianza kushuhudiwa mnamo miaka ya sitini wakati ugonjwa huo ulitangazwa kuwa sugu dhidi ya dawa ya chloroquine kwenye eneo laMekong na kusambaa hadi Afrika ambapo vifo vinavyotokana na Malaria viliongezeka hasa miongoni mwa watoto.

Mkurugenzi wa programu ya malaria ya WHO Robert Newman anasema kuwa kusambaa kwa aina sugu ya ugonjwa wa malaria ni kama janga akiongeza kuwa lazima jitihada zifanywe kukabilina na tatizohilo.