Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa UM wa masuala ya kibinadamu Somalia azuru Bosasso

Mratibu wa UM wa masuala ya kibinadamu Somalia azuru Bosasso

Mratibu mpya mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Philippe Lazzarini ambaye anazuru Somalia kwa mara ya kwanza tangu kushika wadhifa huo mapema mwezi huu amezuru mji wa Bosasso Kaskazini Mashariki mwa Puntland siku ya Jumanne.Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Bwana Lazzarini alilakiwa na maafisa wa serikali, maafisa kutoka wizara ya afya na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa mjini Bosasso.

Bosasso ni makazi ya idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani katika majimbo ya Puntland.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano na viongozo Lazzarini amesema ziara yake inajikita katika hali ya kibinadamu nchini humo na mazingira wanaoishi wakimbizi wa ndani.