Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuisaidia Uchina kuondosha chembechebe zinazoathiri tabaka la ozoni

UM kuisaidia Uchina kuondosha chembechebe zinazoathiri tabaka la ozoni

Bodi ya Umoja wa Mataifa ambayo imeundwa kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na chembembe zinazoathiri tabaka la Ozoni, imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 380 kuisaidiaChinaili kuondosha mazalia ya bidhaa za viwandani zinazotishia tabaka la Ozoni nchini humo .Masalia hayo ambayo yanaunda chembechembe zinazojulikana kitaalamu HCFCs, yanaweza kuondosha tabaka la Ozoni ifikapo mwaka 2030kamahayashughulikiwa sasa. Grace Kaneiya anaarifu

(RIPOTI YA KANEIYA)

China ambayo inaongoza kwa uzalishaji na utumiaji wa HCFCs, inategemea kutokomeza kabisa uzalishaji wa bidhaa hizo, ikiwemo akiba ambayo hadi sasa haijatumika.

Hatua yaChinani sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya kimataifa yanayokwenda sambamba na Itifaki yaMontrealna imehaidi kuondosha kabisa masalia ya chembechembe hizo ifikapo mwaka 2030.

Serikali yaChinainasema kuwa kiasi chachembechembe za HCFCs kinachotakiwa kuondolewa ifikapo mwaka 2030 kitasaidia kuzuia gesi chanfu ya viwandani na takriban tani bilioni 8 za gesi ya carbon dioxide ambayo ni sawa na gesi chafu ya viwandani.

Mara nyingi magadi ya HCFCs hutumika kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo pia kugandisha vitu na masuala ya uzimaji wa motokamambinu mbadala ya kukabiliana na hali upoteaji wa tabaka la Ozoni.