Madhara ya tetemeko la ardhi Uchina yabainika zaidi: OCHA

23 Aprili 2013

Yapata watu mia mbili wamekufa na wengine zaidi ya elfu kumi na mbili wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi  lenye uharibifu mkubwa lililolikumba eneo la Lushan katika jimbo laSichuannchiniChinaApril 20. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kratibu wa Misaada ya Kibinadamu, OCHA, wakati vifo na majeruhi hao wakiripotiwa maeneo mengi hayafikiki na takwimu hizo zaweza kuongezeka wafanyakazi wa uokozi wanapojaribu kufika kwenye maeneo husika.

Licha ya kwamba serikali yaChinahaijaomba msaaada, Umoja wa Mataifa umesema uko tayari kusaidia pale panapohitajika wakati huu ambapo ripoti zinasema zaidi ya watu milioni moja na nusu wameathirika, wengine karibu laki mbili na nusu wakiwa wameshaondolewa kwenye eneo la maafa.

Barabara na madaraja katika eneohiloyameharibiwa vibaya au kufungwa, na zaidi ya askari na wanajeshi 29,000 wameandaliwa kutoa huduma za misaada ya kibinadamu.Jens Laerke ni msemaji  wa OCHA.

 (SAUTI YA JENS LAERKE)

 "Mamalaka za kitaifa ikiwamo wizara ya maswala ya raia wameitikia kwa haraka kwa ugawaji wa misaada kama vile mahema, vitanda, vyajkula na maji ya kunywa katika mji wa Yaang ambao ni mji ulioko karibu katika jimbo hilo , kundi la matabibu na magari ya dharura pia vimeagizwa kuhudumia majeruhi kufuatia tetemeko. "

Shirika la Kuhudumia Watoto la UNICEF limesema zaidi ya watoto 26, 000 katika jimbo la Lushan wameathirika vibaya mno na tetemekohilo.