Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM lawasafirisha raia wa Sudan Kusini wanaarudi nyumbani

IOM lawasafirisha raia wa Sudan Kusini wanaarudi nyumbani

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaendelea na huduma ya kuwasafirisha kwa njia ya ndege zaidi ya raia 700 wa Sudan Kusini ambao wamekuwa wakisubiri kusafirishwa kwenda kwa jimbo laUpper Nilenchini  Sudan Kusini. Joseph Msami na taarifa kamiliWatu hao ni sehemu ya kundi la watu 1,030 waliosafirishwa na kanisa la Inland Church kutoka mji mkuu waSudan Khartoum kwenda Malakal nchini Sudan Kusini.

Hao ni kati ya takriban watu 40,000 wanaoishi kwenye mahema mjiniKhartoum.

Hali kwenye maeneo haya inasalia kuwa mbaya wakati watu hao wakiwa wanakabiliwa na uhaba wa chakula , maji , huduma za afya na usafi. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)