Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waendesha mafunzo kwa maafisa wa serikali ya Somalia

Waendesha mafunzo kwa maafisa wa serikali ya Somalia

Kundi la wataalamu ambao walikwenda ughaibuni na hatimaye kurejea nyumbani Somalia limemaliza awamu yake ya kwanza ya utoaji mafunzo kwa maafisa wa serikali.

Kundi hilo lenye wataalamu saba, lilirejea mjini Mogadishu na kuanzisha mafunzo yanayofahamika kama mafunzo kwa wakufunzi linaendesha kampeni ya kuwajengea uwezo maafisa wa serikali

Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa kwa ushirikiano wa pamoja Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM,na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP.

Mmoja wa wakufuzi kwenye mafunzo hayo amesema kuwa, kutolewa kwa elimu hiyo kutawasaidia maafisa wa serikali kukabiliana na changamoto za kiutendaji wanazokumbana nazo.