Timu ya wataalamu wa UM yahitimisha tathimini ya kinu cha nyuklia cha Japan

22 Aprili 2013

Licha ya mafanikio kadhaa Japan inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa na ngumu wakati huu ikijitahidi kufunga kinu chache cha nyuklia kilichoathirika vibaya na tetemeko la ardhi na Tsunami Machi 2011.Tamko hilo limetolewa na wataalamu kutoka shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA ambao Jumatatu wamehitimisha tathimini ya awali ya juhudi za kukifunga kinu chake cha nyuklia cha Fukushima Daiichi

Wajumbe 13 wa tume hiyo walikuwa Japan tangu April 15 hadi leo April 22 na walizuru mtambo huo ili kujionea hali halisi na kupata taarifa halisi za hatua zilizofikiwa katika.

Ripoti ya awali ya timu hiyo imewasilishwa kwa serikali ya Japan Jumatatu huku ripoti ya mwisho itatolewa ndani ya mwezi mmoja.