Balozi Mahiga alaani mauaji ya mwandishi wa habari Somalia

22 Aprili 2013

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa kwa ajili ya Somalia Balozi Augustine Mahiga amestushwa na kuhuzunishwa na tukio la jana jioni la kupigwa risasi na kuuawa kwa mwandishi wa habari Ibrahim Rageh, aliyekuwa akifanya kazi na Radio yaMogadishuna Televisheni ya Taifa.Balozi Mahiga amelaani kitendo hicho na kutaka watekelezaji wa mashambulizi hayo ya kushtukiza kufikishwa katika vyombo vya sheria huku akizipa pole familia, marafiki na tasnia ya habari nchiniSomalia kufuatia mauaji hayo ya nne kwa wanahabari tangu kuanza mwaka huu ambapo mwaka jana waandishi wa habari 18 waliuwawa.

Hata hivyo amesema waandishi wa habari wataendelea kufanya kazi zao alizoziita uti wa mgongo katika kulinda amani na demokrasia endelevu.

Balozi Mahiga pia amesema jamii ya kimataifa iko upande wao na iko tayari kusaidia serikali katika juhuidi zake za kukomesha ukwepaji wa sheria