Ban ahuzunishwa na hasara iliyosababishwa na tetemeko la ardhi nchini China.

22 Aprili 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kuhuzunishwa kwake kutokana na vifo , majehara na uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi lililolikumba jimbo la Sichuan nchini China mwishoni mwa juma akisema kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada unaohitajika.Kulingana na vyombo vya habari tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 6.6 hadi 7 kwenye kipimo cha Richa lilisababisha vifo vya karibu watu 200 ambapo watu 8000 walijeruhiwa huku pia lilikisabahisha kuwepo kwa uhaba mkubwa wa maji ya kunywa.

Kupitia kwa msemaji wake Ban ametuma rambi rambi zake kwa serikali ya China kwa watu wake hasa kwa wale waliowapoteza wapendwa wao au wale walioathiriwa kwa njia moja na janga hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter