Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapata ripoti kuhusu hali ya Sahara Magharibi

Baraza la usalama lapata ripoti kuhusu hali ya Sahara Magharibi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limefanya mashauriano kuhusu Sahara Magharibi ambapo limepatiwa ripoti kuhusu hali ilivyo kwenye eneo hilo.Ripoti hiyo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na mambo mengine imeeleza kuwa hali ya usalama si mbaya sana na kumekuwepo na maandamano ya hapa na pale ya wananchi wakitoa madai mbali mbali ikiwemo kupokwa kwa rasilimali za nchi hiyo.

Katibu Mkuu amesema mzozo wa Sahel upatiwe suluhu haraka kama sehemu ya kuweka utulivu huko Sahara Magharibi.

Katika ripoti yake ameomba kuongezwa kwa muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sahara Magharibi MINURSO kwa mwaka mmoja zaidi hadi tarehe 30 mwezi Aprili mwakani ili kusimamia utulivu na amani.